Watumishi wapya wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) wameanza kupatiwa mafunzo yanayolenga kuwakaribisha rasmi katika utumishi wa umma, ambapo wamekumbushwa kuhusu masuala muhimu kama maadili, nidhamu, na uwajibikaji kazini. Msajili wa Bodi, Eng. Bernard Kavishe, ametoa wito kwa watumishi hao kuzingatia viwango vya juu vya maadili na kujitolea katika majukumu yao. Semina hii ya mafunzo inafanyika kwa siku tatu, kuanzia tarehe 2 hadi 4 Oktoba 2024, na inalenga kuwajengea msingi imara watumishi wapya ili waweze kutimiza malengo ya Bodi kwa ufanisi.