KAMATI YA PAC YAIPONGEZA ERB KWA UTENDAJI

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) imeipongeza Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kwa utendaji bora. Hayo yamebainishwa na wajumbe wa kamati hiyo wakati Bodi ilipowasilisha taarifa ya utendaji wake kwa mwaka wa fedha 2023/2024 katika Ofisi za Bunge leo, tarehe 9 Novemba 2024.
Msajili na Mtendaji Mkuu wa ERB, Mhandisi Bernard Kavishe amewasilisha taarifa hiyo mbele ya kamati, ambayo imejumuisha sehemu kuu nne ikiwemo majukumu ya Bodi, mafanikio yaliyopatikana, Programu za Uendelezaji wa Wahandisi, na malengo ya baadaye ya Bodi.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mheshimiwa Japhet Asenga (Mb), amesema kwamba ERB imekuwa mfano mzuri wa kuigwa na Bodi nyingine. Aliongeza kuwa taarifa ya utendaji wa Bodi imeonesha wazi mafanikio yake na mikakati yake ya baadaye. “Natamani taasisi nyingine zinazofanya majukumu ya Bodi kuiga mfano wa ERB. Taarifa hii ni nzuri na imeainisha mambo muhimu katika utendaji wake,” alisisitiza Asenga.
Uwasilishaji wa taarifa