Watumsihi ERB Wakumbushwa Maadili, Ufanisi Kazini na Uzalendo

Kikao cha Wafanyakazi wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kimefanyika tarehe 15 Novemba, 2024 katika ukumbi wa St. Gasper jijini Dodoma.
Kikao hiki ni sehemu ya utaratibu wa Bodi wa kufanya vikao vya mara kwa mara ili kuwakumbusha wafanyakazi na kuwajengea uelewa kuhusu masuala mbalimbali ya kiutumishi.
Katika kikao hicho, Msajili na Mtendaji Mkuu wa ERB, Mhandisi Bernard Kavishe, amewataka watumishi kuzingatia maadili na nidhamu katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Aidha Mhandisi Kavishe amewataka watumishi kujiendeleza kimasomo na kuongeza weledi ili kufikia malengo ya taasisi kwa ufanisi zaidi. Kwa upande mwingine watumishi wametakiwa kuwa wazalendo ili kuwa na fikra za kujenga kwa lengo la kuisaidia taasisi kufikia mafanikio.

Kwa upande mwingine, watumishi wamepata fursa ya kujifunza kuhusu namna ya kuvaa kwa staha katika maeneo ya kazi, na jinsi ya kutambua na kukabili matatizo ya afya ya akili maeneo ya kazi.
Watumishi wameshukuru uongozi wa Bodi kwa kuendelea kuandaa vikao vya aina hii, kwani vimekuwa na mchango mkubwa katika kujenga umoja na mshikamano katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku na kuboresha utendaji kazi na kujenga timu imara ndani ya ERB.