Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Mwajuma Waziri, alisisitiza umuhimu wa kuimarisha Chuo cha Maji, si kwa chuo pekee bali pia kushiriki kikamilifu katika shughuli mbalimbali za wizara. Aliongeza kuwa utoaji wa PDU's ni muhimu ili kuvutia ushiriki wa watu wengi zaidi. Mhandisi Mwajuma alitoa kauli hiyo alipotembelea banda la Bodi ya Usajili wa Wahandisi wakati wa kufunga Kongamano la Nne la Kimataifa la Sayansi ya Maji, lililofanyika tarehe 20 Januari 2025, katika Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.