Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ECI) kutoka nchini India Dkt. Priya Ranjan Swarup, awasili Tanzania

Msajili wa Bodi ya Wahandisi (ECI) kutoka nchini India Dkt. Priya Ranjan Swarup, akiwa pamoja na ujumbe wake wamewasili nchini Tanzania na kupokelewa na wenyeji wao kutoka Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kwa ajili ya ziara rasmi leo Februari 10, 2025 Mkoani Dar es Salaam.
Dkt. Swarup atafungua rasmi Semina ya 18 ya utangulizi kwa wahandisi 362 waliojiandikisha katika Mpango wa Mafunzo kwa vitendo (SEAP) pamoja kupata fursa ya kuzungumza na wahandisi wahitimu wapya tarehe 11 Februari, 2025 katika Ukumbi wa PSSS Commercial Complex, Sam Nujoma jijini Dar es Salaam.
Taasisi ya ECI ni chombo kikuu kinachosimamia taaluma ya uhandisi nchini India, kikiwa na jukumu la kuhakikisha viwango vya juu vya ubora wa kitaaluma ambapo moja ya malengo yake ni kusaidia kutambulika kimataifa kwa wahandisi na kuongeza fursa za maendeleo ya taaluma ya uhandisi katika maeneo mbalimbali duniani, ikiwemo Tanzania.