ERB, ECI WAANZA UTEKELEZAJI WA MAKUBALIANO YA KUONGEZA UFANISI KWA WAHANDISI.

Bodi ya Usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) na Baraza la Uhandisi la India (ECI) wameanza utekelezaji wa makubaliano kati yao ambayo yalisainiwa mwezi Disemba 2024 lengo kuu likiwa ni kuchangia maendeleo ya kiuchumi ya nchi hizo.