Kikao kazi cha wafanyakazi kimefunguliwa leo tarehe 18/02/2025 na Msajili

Msajili wa Bodi ya Wahandisi, Mhandisi Bernard Kavishe, leo tarehe 18 Februari 2025, amefungua na kuongoza kikao kazi cha wafanyakazi wa Bodi hiyo kilichofanyika katika ofisi za Bodi zilizopo Dodoma, kwenye Jengo la Mhandisi Annex, ghorofa ya kwanza. Kikao hiki kinalenga kuwapatia wafanyakazi ujuzi na maarifa muhimu katika nyanja mbalimbali katika utekelezaji wa majuku ya kila siku.
Miongoni mwa masuala jadiliwa ni mbinu bora za utunzaji wa nyaraka na kumbukumbu pamoja na elimu ya jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto, ambayo yametolewa na maafisa kutoka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji. Kikao kazi hicho cha siku tatu, pia kitajumuisha zoezi la upimaji wa afya kwa wafanyakazi wote, ili kuhakikisha wanakuwa na afya njema inayochangia ufanisi wao kazini.
Huu ni utaratibu ERB kuandaa vikao vya wafanyakazi, kwa lengo la kuboresha ufanisi na kuwawezesha wafanyakazi kupata elimu ya kina pamoja na ujuzi unaohitajika katika kutekeleza majukumu yao kikamilifu.