NORWAY KUENDELEA KUWEZESHA WAHANDISI WANAWAKE NCHINI

Balozi wa Norway nchini Tanznaia, Bi. Tone Tinnes amesema nchi ya Norway itaendelea kuunga mkono wahandisi kutokana na umuhimu wao katika kuinua uchumi wa nchi, Balozi Tinnes, amesema uchumi wa taifa la Norway umekuzwa na wahandisi baada ya kubadili maporomoko ya maji na kufanya kuwa nishati ya umeme na mbolea, ambapo baadae pia katika miaka ya 70 waligundua gesi na mafuta ambayo pia iliendelezwa na wahandisi.
Ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya 19 ya vitendo kwa wahandisi wahitimu, mafunzo ambayo yanajulikana kwa jina la SEAP, mpango ambao umeanza mwaka 2003. Mafunzo hayo hutolewa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB) kwa kuwapatia wahandisi wahitimu kufanya mafunzo ya vitendo kwa kipindi cha miaka mitatu.
“kupitia mradi huu wa SEAP mpaka sasa tumedhamini kwa takribani miaka 15,na lengo letu ni kuona wahandisi wanawake wanaongezeka ,ili kuwe na uwiano wa kijinsia katika fani hiyo. Amesema balozi Tinnes.