WAHANDISI WAHITIMU WAHIMIZWA KUZINGATIA MAADILI

Kaimu Msajili wa Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), CPA. Paul Bilabaye, amewataka wahandisi wahitimu wanaoshiriki mafunzo ya vitendo kupitia programu ya SEAP, kuhakikisha wanazingatia miiko na maadili ya taaluma yao wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.
CPA Bilabaye ameyasema hayo wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku tatu,ambapo ameeleza kuwa taaluma ya uhandisi ina miiko yake,hivyo ni wajibu wao kuhakikisha wanajitofautisha katika utendaji wao ukilinganisha na wale wanaofanya kazi hizo.