KATIBU TAWALA WA MKOA WA GEITA ATEMBELEA BANDA LA ERB GEITA.

KATIBU TAWALA WA MKOA WA GEITA ATEMBELEA BANDA LA ERB GEITA.
Katika maonesho ya MAT BUILDERS’ EXPO 2025,
Kaimu katibu tawala wa mkoa wa Geita Charles Chacha, ametembelea banda la Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), katika maonesho ya MAT BUILDERS’ EXPO 2025 yanayoendelea katika Mkoa wa Geita katika viwanja vya Samia Suluhu Hassan Bombambili katika Manispaa ya Geita.
Akiwa katika banda la ERB Chacha ametoa msisitizo kwa bodi kutembelea katika miradi mikubwa inayotekelezwa katika mkoa huo,ili ERB ihakikishe miradi hiyo inatekelezwa kwa viwango na kwa ubora unaohitajika.
Katibu Tawala Chacha pia amefungua maonesho hayo rasmi ya MAT BUILDERS’ EXPO 2025 ambayo yanaendelea katika mkoa huo,huku kilele chake ikitarajiwa kuwa tarehe 27 Mei 2025.