STEM MKOA WA GEITA

Bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) imeendelea kutoa huduma zake katika mikoa ya kanda ya ziwa ikiwemo Mwanza,Geita,Mara na Kagera.
Wakiwa mkoani Geita Maafisa wa ERB wakiongozwa na msajili wa bodi ya Wahandisi (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe, wakiambatana na viongozi wa elimu wa wilaya ya Geita, wametembelea shule mbili za za sekondari za Wasichana, Nyankumbu ,pamoja na shule ya sekondari ya Geita. Geita Girls ni shule mpya, miongoni mwa shule kubwa 26 za mama Samia, shule hizi zimejengwa kila mkoa, za sahansi, mahsusi kwa wasichana.
Bodi hiyo metembelea katika shule hizo kwa lengo la Kuchagiza ufundishaji na usomaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati (STEM), kwa msisitizO maalumu kwa wasichana bila kuwaacha wavulana nyuma.
“Sayansi na Hisabati ndio mbegu inayootesha mti wa uhandisi, ndio msingi ambao nyumba ya uhandisi inajengwa” Amesisitiza Msajili wa bodi ya wahandisi, Mha. Bernard Kavishe