KAZI ZA KIHANDISI KWENYE SGR ILIVYORAHISISHA UTALII MIKUMI

KAZI ZA KIHANDISI KWENYE SGR ILIVYORAHISISHA UTALII MIKUMI
Safari kuelekea katika hifadhi ya taifa ya mikumi mkoani Morogoro,safari hii imelenga kuonesha ni kwa kaishi gani kazi za kihandisi inavyochechemua sekta zingine,
Jijini Dar es salaam, katika stesheni ya MAGUFULI,kituo cha kupandia treni ya mwendo kasi,SAFARI inaanzia hapa kwa kushughudia kazi nzuri iliyotukuka iliyofanywa na wahandisi katika ujenzi wa jengo hili la kisasa,
Bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) imeandaa safari ya utalii kuelekea katika hifadhi ya taifa ya Mikumi,lengo likiwa ni kuonesha ni kwa kiasi gani SGR ambayo ni zao la kazi za kihandisi,ilivyo rahisisha usafiri.
Kazi hii ya kihandisi kwa hakika imeleta mapinduzi makubwa katika uchumi ikiwemo kuongeza hamasa ya utalii.
Katika hifadhi ya taifa ya mikumi kila aliyefika hapa hakusita kueleza umuhimu wa treni ya SGR katika kurahisisha utalii katika hifadhi hii ya taifa ya mikumi,na vivutio vingine katika ukanda huo.
Bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) wanasema huu sio mwisho,bali ni mwendelezo wa kuhamasisha shughuli za utalii kwa wazawa na wageni kupitia SGR .