YOUTH ACCELERATION PROGRAM

Mtendaji wa mkuu wa bodi ya mfuko wa barabara Mhandisi Rashid Kalimbaga, amesema bodi hiyo itaunga mkono mpango wa Youth acceleration program,mpango ulioanzishwa na bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) kwa lengo la kuwasaidia vijana kujitambua kwa kunoa bunifu na taaluma zao ili waweze kuanzisha biashara zao wenyewe.
Mhandisi Kalimbaga ameyasema hayo katika kongamano la vijana katika Sayansi na Teknolojia 2025 (Youth in science and technology summit 2025), lililoandaliwa na taasisi ya SERIS kwa kushirikiana na bodi ya usajili wa wahandisi (ERB).
“Nawasisitiza vijana kuwa sio rahisi, lakini inawezekana,na sera ya wizara ya ujenzi ni kuwawezesha vijana kutekeleza miradi ya ndani kwani kwa kufanya hivyo itasaidia taifa kubakiza fedha za ndani ya nchi badala ya kutumia wataalam kutoka nje”amesema Mhandisi Kalimbaga
Pia ameeleza kuwa vijana wa kitanzania wakishakuwa wahandisi,wabunifu,wakadiria majenzi na washauri wa miradi wazuri hakutakuwa tena na haja ya kuwachukua wataalam kutoa nje.
Awali msajili wa bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) ,Mhandisi Bernard Kavishe amesema licha ya vijana hao kufundishwa masula mabalimbali kuhusu uanzishwaji wa biashara zao ikiwemo namna ya kubuni mawazo ya biashara na uandishi wa andiko la mradi,ERB itaendelea kuwalea vijana watakao andika miradi kwani elimu hiyo haina mwisho.
Mhandi Kavishe pia amewataka vijana hao kujiweka sawa kukabili soko la kimataifa kwa kujifunza lugha za kigeni ikiwemo lugha ya kingereza kwani kwenye soko la dunia lugha hiyo haikwepeki.
“Nili kwenda kwenye moja ya nchi ya umoja wa Ulaya,na Amerika nimebaini kuwa kuna uhaba mkubwa wa Wahandisi, wataalam wa afya na wataalam wa lishe,Watanzania wanahitajika huko,kwahiyo vijana wa Kitanzania lazima muwe na sifa ya kufikia soko hilo”. Ameeleza Mhandisi Kavishe.
Kongamano la Vijana katika Sayansi na Teknolojia 2025 (Youth in science and technology summit 2025),bado linaendelea jijini Dar es Salaam katika Ukumbi wa PSSSF commercial Complex ambapo vijana kutoka sehemu mbalimbali wanapata elimu ya namna ya kubuni, kuandika maandiko miradi pamoja na kuendeleza bunifu zao.