MCHANGO WA WAHANDISI NA TEKNOLOJIA MPYA KATIKA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO BUSISI

Msajili wa bodi ya usajili wa wahandisi (ERB) Mhandisi Bernard Kavishe amesema daraja la J.P.MAGUFULI ni daraja lenye viwango vya nyota Tano,kutokana na Daraja hilo kujengwa kwa viwango vya Kimataifa,iwemo kuwa na uwezo wa kupunguza ajali,kujengwa na wahandisi wenye viwango vya kimataifa ,pamoja na matumizi ya teknolojia za kisasa.
"Daraja hilo lina njia mbili za kwenda na njia mbili za kurudi ,na njia hizo zimetenganishwa hivo kutokea kwa ajali katika daraja hilo uwezekano ni karibia 0%,Pia daraja hilo inatambulika kimataifa kwa kuwa daraja la sita kwa urefu barani Afrika.".
Amesema Mhandisi Kavishe wakati akizungumza na waandishi wa habari katika daraja hilo litakalozinduliwa leo na rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.