AEQSRB ZANZIBAR WATEMBELEA OFISI ZA DODOMA

Bodi ya usajili wa Wasanifu, Wahandisi na Wakadiriaji Majengo (AEQSRB) kutoka Zanzibar wamewasili katika ofisi za Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), Dodoma siku ya leo tarehe 21 Agosti, 2025 kwa lengo la ziara ya siku mbili jijini Dodoma. Lengo la ziara hiyo ni kuimarisha ushirikiano pamoja na kufuatilia utekelezaji wa makubaliano na kubadilishana uzoefu katika uendeshaji wa bodi zote mbili. Aidha ziara hiyo inahusisha utembeleaji wa miradi mikubwa ya Ujenzi, ikiwemo mji wa Serikali Mtumba, ujenzi wa kiwanja cha ndege Msalato na ujenzi wa barabara ya mzunguko (ring road). Ziara hiyo imeongozwa na Arch. Nassir Da-Costa na Mrajis, Mhandisi. Mansur Mohamed, ambapo katika ofisi za ERB Dodoma walipokelewa na mwenyeji wao Msajili Msaidizi Uendelezaji Wahandisi, Mhandisi Veronica Ninalwo aliyemwakilisha Msajili wa Bodi, ERB.