SOPEL MOROGORO

Kikao cha tathmini ya utendaji wa Shule ya Uhandisi Mahiri na Uongozi (SoPEL) kimefanyika leo, tarehe 6 Oktoba 2025, katika ofisi za shule hiyo zilizopo Morogoro, ambazo pia ni ofisi za ERB mkoa wa Morogoro. Kikao hicho kilijadili na kuwasilisha ripoti ya tathmini ya utendaji pamoja na mafanikio yaliyopatikana hadi sasa tangu shule hiyo ianze rasmi mwaka jana. Kikao hicho ni sehemu ya utaratibu wa Bodi kuhakikisha kuwa shule hiyo, ambayo ina mchango mkubwa kwa maendeleo ya wahandisi, inafikia malengo na kusudi lililokusudiwa kuanzishwa kwake.