ERB, IMESHIRIKI MBIO ZA CRDB MARATHON

ERB imeshiriki mbio za CRDB Marathon kama sehemu ya maandalizi kuelekea mbio za ERB Marathon Run for STEM. Mbio hizi zina lengo la kuchangisha fedha ambazo zitatumika kulipa posho kwa walimu wanaojitolea kufundisha masomo ya sayansi katika shule za sekondari. Kupitia ushiriki huu, ERB inaonyesha dhamira yake ya kuunga mkono elimu ya sayansi na teknolojia, ikilenga kuimarisha msingi wa taaluma hizo kwa wanafunzi wa sekondari nchini.