ERB MARATHON RUN FOR STEM

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof Adolf Mkenda, ameshiriki mbio za ERB RUN FOR STEM akiwa ni mgeni rasmi wa mbio hizo ambazo zimeanzia viwanja vya UDASA, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. mbio hizo zinalenga kuchangia fedha kwa lengo la kusaidia ufundishaji wa masomo ya sayansi katika shule za sekondari nchini.