ERB MARATHON FOR STEM SASA KUFANYIKA TAREHE 8, SEPTEMBA

ERB MARATHON RUN FOR STEM KUFANYIKA SEPT 8.
Akizungumza na waandishi wa habari msajili wa bodi ya usajili wa wahandisi,Eng.Benard Kavishe amesema Mbio hizo zilikuwa zifanyike Jumamosi hii sasa zitafanyika Jumapili hii septemba 8.
Mhandisi Kavishe amesema malengo ya mbio hizo ni kuunga mkono mradi wa SSP (Stem Support Project) ambao umelenga Kuunga mkono juhudi za serikali ya kuboresha sekta ya Elimu.
Amesema serikali ya awamu ya sita chini ya rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeboresha sekta ya elimu kwa kiasi kikubwa hali iliosababisha kuwepo na uhitaji wa kuongeza walimu hususani wa masomo ya Sayansi.
Kupitia mradi huo ERB tayari imeshaajiri walimu 20 wa masomo ya sayansi ambapo lengo la mbio hizo ni kuongeza fedha kwaajili ya kuajiri walimu wengine.
Mbio hizo zitahusisha kilometa 5,10 na kilometa 21 ambazo zitaanzia na kuhitimishwa katika viwanja wa UDASA CLUB katika chuo kikuu cha Dar es Salaam.