ANNUAL ENGINEERS DAY, 2024

WAHANDISI WATAKIWA KUENDANA NA KASI YA MABADILIKO YA TEKNOLOJIA
Waziri wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ametoa rai kwa Wahandisi nchini kuendana na kasi ya mabadiliko ya Teknolojia mbalimbali ikiwemo ya Akili Mnemba kutoa suluhu ya changamoto mbalimbali zilizopo katika jamii.
Bashungwa ameeleza hayo leo Septemba 05, 2024 wakati akifungua Maadhimisho ya 21 ya Siku ya Wahandisi iliyobeba kauli mbiu “Kuandaa Nguvukazi ya Uhandisi katika zama za Akili Mnemba - Mafunzo na Kuimarisha Ujuzi wa Watalaam wa Kada ya Uhandisi”.
“Tumieni fursa hii kutafakari changamoto mbalimbali za shughuli za kihandisi zenye mahusiano ya moja kwa moja na maendeleo ya nchi yetu, badilishaneni mawazo na kuona ni teknolojia ipi itasaidia kutatua changamoto”, amesema Bashungwa.