WAHANDISI CHANGAMKIENI FURSA ZA UJASIRIAMALI

Wahandisi Vijana nchini wameshauriwa kutumia fursa mbalimbali kupitia ujuzi na ubunifu waliokuwa nao ili kuwa wajasiriamali na kuleta mabadiliko chanya kwao na Taifa kwa ujumla.
Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mhandisi, Zena Said leo, Septemba 4, 2024 wakati akifunga Jukwaa la Wahandisi Vijana jijini Dar es Salaam lililobebwa na kauli mbiu isemayo “Ujasiriamali na Uhandisi, kuongeza Kasi kwa Wahandisi Vijana kufikia Ubora” ambalo limeratibiwa na Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB)